Mheshimiwa Balozi Iman Salum Njalikai,Balozi wa Tanzania nchini Algeria leo tarehe 30 Septemba, 2024 amekutana kufanya Mazungumzo na Prof. Khalid Rouaski, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Algiers 3 nchini Algeria.

Kwa pamoja wamekubaliana fursa ya kuanzisha Ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya Tanzania na Algeria katika eneo la Tafiti,ziara za Wahadhiri na Wanafunzi ikiwa ni pamoja na uandaaji wa Makongamano ya Kitaaluma.