Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Msumbiji nchini Algeria, Mhe. António Namburete, mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Algiers mnamo tarehe 17 Juni, 2026, kwa ajili ya kutambulishana na kuzungumzia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili chini ya mwongozo wa ushirikiano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
