Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Algeria, Mhe. Edward Kwaku Cofie, mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Algiers mnamo tarehe 15 Juni, 2026, kwa ajili ya kutambulishana na kuzungumzia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kupitia balozi zake jijini Algiers.
